villafm

Mashemeji na marafiki wamcharukia Kanye West

  • Home    /
  • Mashemeji na marafiki wamcharukia Kanye West
Mashemeji na marafiki wamcharukia Kanye West

Baada ya mwanamuziki KanyeWest na mkewe Bianca Censori kutokuwa kwenye maelewano mazuri kwa hivi karibuni, marafiki wa mwanamke huyo wanadai kuwa Kanye anamchukulia mkwewe kama mradi wa sanaa.
Marafiki hao kutoka nchini Australia wamefichua kuwa Bianca anafanywa kama mradi wa sanaa na biashara kwa kuvaa mavazi yasiyofaa wakati akiwa na Kanye.
Aidha tovuti ya Times Now imeeleza kuwa baadhi ya watu wanamuona Bianca kama amerukwa na akili kutokana na kufuata sheria za mumewe hasa kwenye mavazi.
Ikumbukwe kuwa rapper huyo mwenye umri wa miaka 46, alimuoa Bianca mwaka 2022, muda mfupi baada ya kuachana na Kim Kardashian.

leave a comment

0 comments

login

author_img