villafm

Usyk amshinda Fury na kuwa bingwa wa dunia

  • Home    /
  • Usyk amshinda Fury na kuwa bingwa wa dunia
Usyk amshinda Fury na kuwa bingwa wa dunia

Tyson Fury alishindwa kwa pointi nchini Saudi Arabia huku Oleksandr Usyk akiwa bingwa wa kwanza wa ndondi za uzani mzito zaidi kushikilia mikanda minne duniani.
Katika usiku uliosheheni ujuzi wa kila aina kutoka kwa mabondia hao Tyson Fury alianza vyema mechi hiyo lakini akaokolewa na kengele katika raunndi ya tisa kutokanna na kichapo cha Usyk.
Akiwa katika hali ya kusubiri kadi za matokeo kusomwa, Fury alionekana kushawishika kupata ushindi kabla ya kadi hizo kumpatia ushindi Usyk
Kadi za matokeo zilisomeka 115-112 na 114-113 kwa raia wa Ukraine, huku jaji wa tatu akifunga 114-113 kwa Fury.
Ilimaanisha Fury, 35, alipoteza kwa mara ya kwanza katika taaluma ya miaka 16. Atapata fursa ya kulipiza kisasi kwa mechi ya marudiano iliyopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

leave a comment

0 comments

login

author_img

Copyright © 2024 Villa Fm Developed by Villa Fm.

Adonis Music R&B